Lema afikishwa Mahakamani

Lema afikishwa Mahakamani kwa makosa ya Uchochezi, aachiwa kwa dhamana!

Hali ya mji wa Arusha ni Kijibaridi na kumekucha kwa manyunyu,Watu wamekuwa ktk vikundi huku usafiri ukidaiwa kuwa wa taabu katika baadhi ya maeneo kutokana na wengi kuja kufuatilia Mashitaka dhidi ya Mbunge wa Arusha Mjini Kamanda Godbless Lema...

Nipo hapa clocktower naelekea mahakamani.Pamoja nanyi naitwa Julius George nitakuwa na makamanda wengi kukuletea LIVE COVERAGE:

Quote By Mungi View Post
Tupo ndani ya ukumbi wa mahakama, kamanda Lema yupo ndani ya ukumbi, yupo pia Nassari pamoja na Amani Golugwa katibu wa mkoa.
Kamanda Lema wanabadilishana mawazo na Wakili Humphrey Mtui na Nassari. Kwa nje ni nyomi ya watu
Quote By Nanyaro Ephata View Post
Ndio shughuli za mahakama inaanza. Mh Godbless Lema anatetewa na Wakili Kimomogoro na Humphrey Mtui.
Quote By Mungi View Post
Tayari hakimu Joyce Msofe ameingia, mahakama imeanza. Anasimama Wakili Method Kimomogoro anajitambulisha.

Hakimu: Hili ni shauri jipya, naomba lisomwe kama inavyostahili.

Lema unashatkiwa kwa kosa moja kinyume na sheria, ulichochea wanafunzi wa chuo cha uhasibu, na kumzomea mkuu wa mkoa kama ifuatavyo, uliwaambia wanafunzi kuwa mkuu wa mkoa hajui chuo cha uhasibu ilipo, na amekuja akiwa amechelewa, anaingia hapa kama anaingia kwenye send off.
Quote By Mungi View Post
Lema amekana kosa, na mwendesha mashtaka amesema dhamana lipo wazi kama atatimiza masharti ya dhamana. Taratibu za dhamana ndo inaanza sasa. Kesi itapangiwa tarehe nyingine pending investigation.
Quote By Mungi View Post
Kesi imeahirishwa mpaka tarehe May 29.
============================== ============================== =
PICHA: Ndugu Godbless Lema akiwa mahakamani NA akiwa anatoka Mahakamani
============================== ============================== =
source Jamii  Forum




Moja ya mabango ya wadau walio kuwa nje

SPORTS BOX

Phasellus facilisis convallis metus, ut imperdiet augue auctor nec. Duis at velit id augue lobortis porta. Sed varius, enim accumsan aliquam tincidunt, tortor urna vulputate quam, eget finibus urna est in augue.

No comments: