Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kimesema hakitakubali
kuzibwa midomo bungeni kwa ajili ya kupigania haki za Watanzania.
Hivi karibuni wabunge watano wa Chadema walifukuzwa bungeni na kupewa
adhabu ya kutohudhuria vikao vitano vya Bunge la Bajeti kutokana na
madai ya kufanya vurugu.
Mwenyekiti wa Chadema Taifa, Freeman
Mbowe, aliyaeleza hayo jana wakati akizungumza na maelfu ya wananchi wa
kata ya Ruaha wilayani Kilosa mkoani hapa kwa kusema hawatishwi na hali
hiyo kwakuwa tayari Watanzania wamewaelewa wabunge wa chama hicho ndiyo
watetezi wa maslahi yao.
“ Kuna upendeleo wa wazi unafanyika
pale bungeni lakini nyinyi Watanzania mnajua wabunge wa Chadema ndiyo
wanatetea maslahi yenu hivyo wanatafuta sababu ya kutupunguza nguvu
lakini tunawaambia hawataweza kutuziba midomo tutaendelea kuwatetea tu,”
alisema Mbowe na kushangiliwa na umati mkubwa watu.
Alisema
namna Chadema inavyojitahidi kutetea haki za Watanzania kupitia kwa
wabunge wake ni pamoja na kuhakikisha hotuba za mawaziri vivuli wa chama
hicho zinazowasilishwa bungeni wanaidurufu na kusambaza kwa wananchi wa
ngazi za chini hasa kuanzia ngazi za vijiji ili waone viongozi wao
wanachokifanya.
Alisema kuwa Chadema itahakikisha inapigania
rasilimali za nchi ili zitumike kwa manufaa ya wananchi wote na sio watu
wachache ambao hawana uchungu na nchi.
“Sisi Chadema hatupo
bungeni kwa ajili ya kuwafurahisha wachache bali ni kutetea haki za
wanyonge hivyo nawaomba Watanzania mtuunge mkono katika juhudi za
Chadema ili kuleta ukombozi,” alisema Mbowe.
Mbowe pia
aliwaombea kura wagombea wa nafasi za mwenyekiti wa kitongoji kata ya
Ruaha huku akiwataka viongozi wa Chadema kufanya kazi kwa uadilifu na
kuwatendea haki wananchi wote bila ya kujali itikadi zao za kisiasa.
Katika mkutano huo wananchi walieleza kero zao mbalimbali ikiwamo suala
la mwenyekiti wa kijiji cha Ruaha, Isaack Maliwa, kupitia Chadema
kuwekwa rumande zaidi ya miezi sita na kukosa dhamana na hivyo
walimuomba Mbowe kupeleka hoja hiyo bungeni ili Watanzania wengine wajue
namna sheria za nchi zinavyokiukwa. CHANZO: NIPASHE JUMAPILI
SPORTS BOX
Phasellus facilisis convallis metus, ut imperdiet augue auctor nec. Duis at velit id augue lobortis porta. Sed varius, enim accumsan aliquam tincidunt, tortor urna vulputate quam, eget finibus urna est in augue.
No comments:
Post a Comment