Idadi ya watuhumiwa wa tukio la kulipua bomu katika Kanisa la Mtakatifu Joseph Mfanyakazi, yaongezeka
Idadi
ya watuhumiwa wa tukio la kulipua bomu katika Kanisa la Mtakatifu
Joseph Mfanyakazi, Parokia ya OLASITI mkoani ARUSHA Jumapili iliyopita
imefikia watu 12.
Watuhumiwa hao wametajwa na Jeshi la Polisi
kuwa ni VICTOR KALISTI na JOSEPH LOMAYANI, ambao wote ni waendesha
bodaboda wakazi wa KWA MROMBO mkoani ARUSHA.
Kamanda wa Polisi
mkoa wa ARUSHA, Kamishna Msaidizi wa polisi LIBERATUS SABAS amewataja
watuhumiwa wengine wanaoshikiliwa kuwa ni GEORGE SILAYO, mfanyabishara
na mkazi wa OLASITI; MOHAMED SAID, mkazi wa ILALA mkoani DAR ES SALAAM,
ambaye ametajwa kuwa ni mwenyeji wa watuhumiwa raia wa Uarabuni.
Wengine wanaoshikiliwa ni SAIDI ABDALLAH SAID, raia wa Falme za
Kiarabu; ABDULAZIZ MUBARAK, mkazi wa SAUDI ARABIA; JASSINI MBARAK, mkazi
wa Bondeni ARUSHA; FOUD AHMED, raia wa Falme za Kiarabu na SAID MOHSEN,
mkazi wa NAJRAN- Falme za Kiarabu.
Jeshi la Polisi nchini kupitia Mkuu wake, Inspekta Jenerali, SAID MWEMA limetangaza donge nono la shilingi milioni 50 kwa mtu yeyote atakayefanikisha kufichua mtandao wa kigaidi nchini.
chanzo CG FM RADIO
SPORTS BOX
Phasellus facilisis convallis metus, ut imperdiet augue auctor nec. Duis at velit id augue lobortis porta. Sed varius, enim accumsan aliquam tincidunt, tortor urna vulputate quam, eget finibus urna est in augue.
No comments:
Post a Comment