| Kalapina kulia akiwa na fan wake |
Baada ya muasisi wa harakati za hip hop Tanzania Kalapina kumchapa
Rapper Chidi Benz katika jukwaa la maisha club alfajiri ya kuamkia leo,
Kalapina ameelezea sababu za kutoa dozi hiyo kwa msanii mwenzake,
namnukuu " ukweli ni mambo fedheha, mdogo wetu chidi benzi cocaine au
heroin / unga anaovuta unampeleka pabaya, tena mimi kama kaka yake
namshauri aachane na matumizi ya madawa kulevya, kwa sababu mwisho wake
utakua m'baya, mimi nilikua back stage na ikafika zamu yangu kupanda
jukwaani nikawa naskia sauti mtu anatamba jukwaani kwa dakika saba ama
nane, alikua ananichelewesha kupanda, na ananiharibia show yangu, huyu
mtu si adui, nikatoa amri mara tatu kama F.F.U aka kaidi ndipo nikamfata
na kumpa dozi, siku akaanguka chini na mimi nikaendelea na show yangu,
hakuna hata mtu mmoja atakaye kubali kuharibiwa kazi, hata rais Kikwete
ukimharibia utaishia jela."
source: XXL/ CLOUDSFM
source: XXL/ CLOUDSFM
No comments:
Post a Comment