Taarifa Na Picha Za Matukio Kwenye Mlipuko Wa Kanisa Arusha
![]() |
| Kanisa La Olasiti |
Kanisa
Katoliki la Parokia ya Olasiti ambalo leo hii lilikuwa linategemea
kupandishwa hadhi na kuwa Parokia limelipuliwa na kile kinachesemekana
kuwa ni bomu na watu wasiojulikana.
Kwa mujibu wa mashuhuda mbalimbali jumla ya watu watatu inasemekana wamefariki mpaka sasa, huku taarifa ya Jeshi la Polisi nchini ikisema ni mtu mmoja tu aambae amethibitishwa kufa kutokana na tukio hilo.
Shuhuda mmoja amesema watu watatu wamefariki na wengine zaidi ya 30 kujeruhiwa vibaya sana, baadhi wakiwa wamekatika viungo vya miili yao.
Nilipoongea na shuhuda mwengine aitwaye Tinah Kivuyo yeye alisimulia juu tukio hilo alivyoliona, "wakati watu wanaingia kwenye ibada huku kukiwa na mkusanyiko mkubwa wa waumini, ghafla bomu lililipuka na kusababisha kifo cha mtu mmoja pale pale na wengine wengi wakiwa ni majeruhi"
Aliendelea
kwa kusema "damu zilitapakaa ikiashiria kuwa watu wengi wamejeruhiwa
vibaya na bomu hilo huku hali zao zikiwa si nzuri, baadhi ya majeruhi
wamekimbizwa kwenye hospitali za Mount Meru, Seriani na St Elizabeth."
Inasemekana
bomu hilo lilirushwa na mtu asiyejulikana, huku watu wengi wakihusisha
tukio hilo na chuki za kidini zinazoendelea kupandikizwa kwa kasi.




No comments:
Post a Comment