Mwanamuziki staa wa Bongo Fleva, Rehema
Chalamila ‘Ray C’ ambaye amepotea katika anga la muziki kwa kipindi
kirefu kutokana na matatizo ya matumizi ya madawa ya kulevya,
amejitokeza akiwa amefutuka.
Hivi karibuni, Ray C ameibuka
na kuanza kutundika picha na vipande vya video zake katika kurasa zake
kwenye mitandao ya kijamii, ikiwa ni sehemu ya kujiweka karibu na
mashabiki wake.
Kufuatia ishu hiyo, kumeibuka mshtuko mkubwa kwa
baadhi ya watu kutokana na picha hizo kumuonesha ‘bidada’ akiwa
amenenepeana ghafla tofauti na alivyozoeleka.
UNENE UNATOKANA NA DOZI?
Baadhi ya mashabiki wake katika mtandao wa Instagram walidai kuwa inawezekana unene huo unatokana na dozi ya kuacha ‘unga’.
Hata
hivyo, wengine walimshukuru Mungu kwa kuwa sasa afya ya mwanadada huyo
inaonekana kurudi katika hali yake ya kawaida tofauti na miezi kadhaa
aliporipotiwa na gazeti hili akiwa amezimika kutokana na matumizi ya
unga.
Katika picha hizo, Ray C anaonekana kufutuka usoni, kifuani na mapajani ambapo awali kabla ya matatizo hakuwa hivyo.
Wengi walimshukuru Mungu kumuona tena Ray C akiwa mzima pamoja na ukimya wake katika muziki.
Ray
C amekuwa akitundika picha hizo kwa ajili ya mashabiki na marafiki hasa
kupitia Instagram akiambatanisha na maelezo huku nyingine zikizungumza
zenyewe.
HATAKI KUTAJA ANAPOISHI
Maelezo ya picha hizo yamekuwa yakielezea maisha ya Ray C kwa sasa akiwa kwenye mjengo wa maana bila kutaja ni sehemu gani.
Kwa
mujibu wa mashabiki wa Ray C, mwanadada huyo kwa sasa anakula bata tu
huku akimshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Jakaya
Mrisho Kikwete ambaye anamuita ‘Daddy’ kwa kuwa ndiye aliyemsaidia
kimatibabu.
Daktari mmoja maarufu jijini Dar aliyehojiwa ,
alibainisha kuwa kinachosemwa na mashabiki wa Ray C kwamba
kinachomnenepesha ni dozi ya kuacha madawa ya kulevya, kinaweza kuwa
kweli au kisiwe kweli.
Aliongeza kuwa kunenepa kunachangiwa na
vitu vingi kama kupata maisha mazuri yasiyohusisha msongo wa mawazo au
mihangaiko ya hapa na pale hivyo anachofanya ni kula, kulala na
kustarehe tu.
Popular Posts
-
Mshambuliaji Alexandre Pato yuko jijini London, England kumalizia mazungumzo kabla ya kujiunga na Chelsea. Raia huyo wa Brazil aliye...

No comments:
Post a Comment