Msanii wa filamu nchini, Dr Cheni amelazwa toka jana katika
hospitali ya Buruhani jijini Dar es Salaam kutokana na ugonjwa wa
Dengue.
Akizungumza nasi leo Dr Cheni amesema kuwa bado hali yake sio
nzuri kutokana na kuishiwa damu na mwili kupoteza nguvu.
“Bado ni nipo
hospitali ya Buruhani naumwa hili gonjwa jipya,sijui unaitwa Dengue,” amesema.
“Bado hali yangu sio nzuri kabisa,yaani naumwa,napungukiwa
damu,mwili unauma,kwahiyo yanai bado ninaumwa,hii homa ilinianzia wiki
iliyopita sema nilikuwa bado hawajaigundua ila jana ndio wameingundua,”
ameongeza.
Dr Cheni amesema kuwa anawaomba Watanzania wamuombee kwani bado
hali yake sio mzuri.
No comments:
Post a Comment