Emmanuel
Adebayor amesaini mkataba wa miezi 18 na Crystal Palace.
Imeelezwa
mkataba huo unatakiwa kuish mwisho wa msimu huu lakini utakuwa na vipindi kama
pande mbili zitakubaliana kuongeza.
Mshambuliaji
huyo mwenye miaka 31, raia wa Togo aliendelea kubaki kwa huku akisubiri dirisha
dogo lifunguliwe.
Lakini
wakati huo Spurs iliendelea kumlipa pauni 100,000 kwa wiki kama mkataba wake
ulivyokuwa ukisema.
Mkataba
wake na Spurs unaisha Juni, mwaka huu lakini klabu hiyo inatakiwa kuendelea
kumlipa hadi Septemba, mwaka huu.
Baada
ya Arsenal, Manchester City na Spurs, Adebayor anaichezea Palace kama klabu
yake ya nne katika Ligi Kuu England.
Pia
amewahi kukipiga katika klabu ya Real Madrid iliyokuwa chini ya Jose Mourinho.


No comments:
Post a Comment