shirikisho
la soka la soka duniani (fifa) limefuta adhabu iliyokuwa inavikabili vilabu vya
real madrid na atletico, ambapo kwa sasa ziko huru kwa usajili hadi hapo
zitakapo sikilizwa rufani zao na shirikisho hilo.
klabu
zote mbili ziliandika katika taarifa zao kuwa fifa imeziachia huru kuendelea na
usajili wa wachezaji mara baada ya kufungiwa kufanya hivyo kutokana na kufanya
usajili wa watoto, kinyume na utaratibu.
real
madrid na atletico zote ziliwasilisha rufani zao kwa shirikisho hilo na sasa zitaendelea
kuwa huru hadi hapo fifa itakapopitia upya kesi zao na kufanya maamuzi.
adhabu
kama hiyo iliikumba klabu ya barcelona mwaka 2014 na kushindwa katika rufaa
yao, kitu kilichopelekea klabu hiyo kusajili wachezaji arda turan na alex
vidal ambao imeanza kuwatumia mwezi huu wa january mara baada ya kumaliza
kifungo.

No comments:
Post a Comment