Nahodha wa Chelsea John Terry anatarajiwa kuihama klabu hiyo mwisho wa
msimu huu mara baada ya kupewa taarifa na uongozi kuwa hatoongezewa
mkataba mpya kuendelea kuichezea klabu hiyo yenye maskani yake Stamford
Bridges.
Terry aliweka wazi taarifa hiyo mara baada ya kumalizika kwa mchezo wa
kombe la FA walipoishinda klabu ya MK Dons magoli 5-1 na kutinga hatua
ya 16 bora, kuwa baada ya kukaa na uongozi wiki iliyopita aliambiwa
kuwa hatopewa mkataba mpya mezani.
Kama ataondoka klabuni hapo, John Terry amesisitiza kutojiunga na klabu
yeyote ile ya ligi kuu nchini England na kwamba anaumia kuondoka kwa
namna hii kwa klabu aliyoihudumia kwa miaka 21 hadi sasa.
Ingawa taarifa ya klabu baadae ikasema kuwa ni kweli kuwa walimtaarifu
John Terry kuwa hatopewa mkataba mpya, lakini kwa kuheshimu huduma ya
nahodha wao huyo wapo tayari kwa mazungumzo na lolote linaweza tokea
katik miezi kadhaa ijayo.
Wachambuzi mbalimbali nchini England wameshangazwa na kitendo hiki cha
kukosa utiifu kwa klabu ya Chelsea dhidi ya wachezaji wake walioisaidia
timu yao kwa maisha yao yote, Jamie Carragher na wachambuzi wengine
wengi wanam-rate John Terry kuwa miongoni mwa mabeki bora zaidi katika
historia ya ligi hiyo.
Popular Posts
-
Mshambuliaji Alexandre Pato yuko jijini London, England kumalizia mazungumzo kabla ya kujiunga na Chelsea. Raia huyo wa Brazil aliye...



No comments:
Post a Comment