GADNER: INGEKUWA SIJAOA NINGEMUOA VANESSA MDEE
MUME wa Legend wa Bongo Fleva, Judith Wambura ‘Lady Jadee’, Gardner G Habash ‘Kapteini’ aliwaacha watu midomo wazi baada ya kusema kama angekuwa hajaoa, basi angemuoa msanii anayekuja kwa kasi kwenye gemu, Vanessa Mdee.
Kapteini alitamka hayo juzi katika kinyang’anyiro cha kumtafuta Redds Miss Dar Indian Ocean 2013 kilichochukua nafasi katika Ukumbi wa Makumbusho ya Taifa, Posta jijini Dar ambapo mume huyo wa Lady Jaydee alikuwa MC wa shughuli hiyo hivyo kutumia kipaza sauti kumnadi Vanesa.
“Kiukweli Vanesa ni msanii mzuri, ana uwezo mkubwa wa kufanya muziki wa Hip Hop na kulitawala jukwaa. Ningekuwa sijaoa kwa kweli ningemuoa Vanesa Mdee,” alisema Gardner.
Mbali na Vanesa, wasanii wengine wanaounda familia ya B Heatz walipata nafasi ya kutumbuiza katika hafla hiyo akiwemo mkongwe, Ally Baucha.
Popular Posts
-
Drogba Mshambuliaji wa zamani wa Chelsea Didier Drogba: hatorudi kujiunga na timu hiyo badala yake ataendelea kubaki ktk klabu ya ...
-
Tajiri mamba moja duniani, Bill Gates leo alitembelea katika mazoezi ya kikosi cha Everton kinachoshiriki Ligi Kuu England. Gates a...
-
Stephan El shaarawy Mshambuliaji nguli wa AC Milan Stephan El Shaarawy amekamilisha uhamisho wake wa mkopo wa kujiunga na miamba mingin...
-
Producer mwenye historia kubwa na ya kipekee katika muziki wa Bongo Fleva P-Funk Majani ameonesha kumuunga mkono Lady JayDee...
-
Arusha. Chadema kimethibitisha umwamba wake katika siasa za Jimbo la Arusha Mjini, baada ya kutetea kwa kishindo kata zake nne kwenye ...
-
Ramires Kiungo wa Chelsea Ramires yuko mbioni kujiunga na klabu ya China inayofamika kwa jina la Jiangsu Suning. Ramires, 28, ali...
-
Listen to Stamina ft Rich Mavoko -Najuta Kubalehe on Hulkshare - Free Music Streaming & Download
-
Klabu ya Real Madrid imekubali kumsajili kiungo Mateo Kovačić kutoka klabu ya Inter Milan ya Italia kwa dau la pauni milioni 21. Mateo mwe...
No comments:
Post a Comment