messi kukutana na yule mtoto aliyeva jezi ya plastic
Star wa klabu ya Barcelona Lionel Messi amepanga kukutana na na ambaye picha yake ilisambaa mitandaoni akiwa amevaa jezi ya mfuko wa plastic .
Juma lililopita kulikuwa na mjadala mkubwa kuhusu ni kijana huyo ambaye amevaa mfuko wa plastic wenye rangi sawa na jezi ya bendera ya timu ya taifa ya Argentina ambao umeandikwa jina la Messi na namba 10 ambayo Messi huvalia akiwa kwenye kikosi cha Argentina.
Picha hiyo inaonesha ni jinsi gani Messi alivyo maarufu duniani na kuwagusa wengi lakini kampeni ya kuanza kumtafuta mtoto huyo ni nani ilianza mara moja kupitia mitandao ya kijamii.
Picha hiyo ilianza kusambaa katikati ya mwezi January lakini baadaye ikafahamika kijana huyo alikuwa ni wa Afghanistan.
Kijana huyo mwenye umri wa miaka mitano anafahamika kwa jina la Murtaza Ahmadi kutoka Afghanistan vijijini.
Jumapili website ya michezo ya Argentina TYC ilithibisha kwamba Messi amezipata picha za Murtaza na amepanga kukutana na kijana huyo.
Murtaza, ambaye anaishi Ghazni, Kusini mwa Afghanistan ameshatafutwa kwa ajili ya kukutana na Messi. Kwasasa bado haijapangwa siku wala saa ambapo pande mbili hizo zitakutana.
Afisa habari wa shirikisho la soka la Afghanistan, Syed Ali Kazemi, ametangaza kwamba: “Uongozi wa Afghan Football Federation (AFF) umepokea email kutoka kwa Lionel Messi na Barcelona kuhusu Messi kukutana na Murtaza”.
Murtaza atatimiza ndoto yake ya kukutana na Leo Messi lakini kuna taarifa inayosema kwamba kijana huyo ni shabiki mkubwa wa Cristiano Ronaldo.
Popular Posts
-
Drogba Mshambuliaji wa zamani wa Chelsea Didier Drogba: hatorudi kujiunga na timu hiyo badala yake ataendelea kubaki ktk klabu ya ...
-
Tajiri mamba moja duniani, Bill Gates leo alitembelea katika mazoezi ya kikosi cha Everton kinachoshiriki Ligi Kuu England. Gates a...
-
Stephan El shaarawy Mshambuliaji nguli wa AC Milan Stephan El Shaarawy amekamilisha uhamisho wake wa mkopo wa kujiunga na miamba mingin...
-
Producer mwenye historia kubwa na ya kipekee katika muziki wa Bongo Fleva P-Funk Majani ameonesha kumuunga mkono Lady JayDee...
-
Arusha. Chadema kimethibitisha umwamba wake katika siasa za Jimbo la Arusha Mjini, baada ya kutetea kwa kishindo kata zake nne kwenye ...
-
Ramires Kiungo wa Chelsea Ramires yuko mbioni kujiunga na klabu ya China inayofamika kwa jina la Jiangsu Suning. Ramires, 28, ali...
-
Listen to Stamina ft Rich Mavoko -Najuta Kubalehe on Hulkshare - Free Music Streaming & Download
-
Klabu ya Real Madrid imekubali kumsajili kiungo Mateo Kovačić kutoka klabu ya Inter Milan ya Italia kwa dau la pauni milioni 21. Mateo mwe...




No comments:
Post a Comment